March 14, 2025
Dear Stakeholder,
Effective Climate Solutions 1 FZCO (“ECCS1”) and its affiliates will implement carbon project activities in Kenya for the proposed Gold Standard Programme of Activities (PoA) ‘Effective Electric dMRV Cooking Solutions Program for Africa’. The proposed projects are being developed with the objective of displacing the use of traditional, low efficiency cookstoves households in Kenya. This will be achieved through the distribution and installation of modern & metered cooking devices (including electric induction cookstoves).
The PoA will be managed by ECCS1 and its appointed affiliates. In this context a series of Local Stakeholder Consultation (“LSC”) live meetings have been planned in Kenya. The LSC meetings will be carried out to gather feedback from all local, affected and interested stakeholders, including non-governmental organizations, women groups, research institutes and organizations/individuals working on topics related to the project activity, policy makers on a national and state level as well as for local people, communities and or representatives who are directly or indirectly affected by the project.
Please note that this Local Stakeholder Consultation would also be valid for any other Voluntary Project Activities (VPAs) implemented later in Kenya under the proposed PoA “Effective Electric dMRV Cooking Solutions Program for Africa’’, provided that the VPAs are homogeneous, i.e. deploy the same stove type(s), target the same end-users and consist of the same project boundary.
ECCS1 invites all interested parties to attend one of the following Local Stakeholder Consultation meetings:
Stakeholders who cannot physically attend the meeting have the possibility to participate online through Zoom. The login details are the following:
Please find attached a Non-Technical Summary of the project.
In case of any questions or for further details and project information prior to the consultation, please write to us via email to:
Jillian Ochoi, Project Manager-Carbon - jillian.ochoi@burnmfg.com
Mpendwa Mdau,
Effective Climate Solutions 1 FZCO (“ECCS1”) na washirika wake wataendesha shughuli za mradi wa kaboni nchini Kenya kwa Mpango wa Shughuli wa Gold Standard unaopendekezwa, unaoitwa ‘Effective Electric dMRV Cooking Solutions Program for Africa’. Mradi huu unapendekezwa kwa madhumuni ya kupunguza matumizi ya majiko ya kienyeji yenye ufanisi mdogo katika kaya za Kenya. Hili litafanikishwa kupitia usambazaji na usakinishaji wa vifaa vya kisasa vya kupikia vinavyopimwa kwa mita (ikiwemo majiko ya umeme ya induction).
Programu wa Shughuli (PoA) utasimamiwa na ECCS1 pamoja na washirika wake walioteuliwa. Katika muktadha huu, msururu wa mikutano ya Mashauriano ya Wadau wa Ndani (“LSC”) umepangwa kufanyika nchini Kenya. Mikutano hii inalenga kukusanya maoni kutoka kwa wadau wote wa ndani, walioathirika, na wenye maslahi, wakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali, vikundi vya wanawake, taasisi za utafiti, mashirika na watu binafsi wanaofanya kazi katika nyanja zinazohusiana na shughuli za mradi, watunga sera katika ngazi ya kitaifa na kaunti, pamoja na jamii au wawakilishi wa jamii wanaoathiriwa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na mradi huu.
Tafadhali kumbuka kuwa mashauriano haya pia yatatumika kwa Shughuli nyingine zozote za Mradi wa Hiari (VPAs) zitakazotekelezwa baadaye nchini Kenya chini ya PoA inayopendekezwa ya ‘Effective Electric dMRV Cooking Solutions Program for Africa’, ikiwa yatazingatia usawa/ uwiano kama wa kuleta majiko ya aina ile ile, itawalenga watumiaji wale wale na itakuwa na mipaka sawa/ ile ile ya mradi.
Mji wa Nyeri
Kwa wadau wasioweza kuhudhuria mkutano wa ana kwa ana, kuna uwezekano wa kushiriki mkutano mtandaoni kupitia Zoom. Maelezo ya kuingia ni kama ifuatavyo:
Zoom: Jiji la Mombasa
Tafadhali pata kiambatisho cha Muhtasari wa Mradi usio wa Kiufundi kwa maelezo zaidi.
Kwa maswali yoyote au maelezo ya ziada kuhusu mradi kabla ya mashauriano, tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe:
Jillian Ochoi, Meneja wa Mradi – Carbon jillian.ochoi@burnmfg.com
Tunatarajia ushiriki wako katika mashauriano haya muhimu kwa maendeleo endelevu ya mradi.
Karibu!