February 11, 2022
Ndugu Mdau,
BURN Manufacturing Co. kwa kushirikiana na Gilbert Solar Energy watautekeleza Mradi wa Hiari (VPAs) chini ya Gold Standard Programme of Activities (PoA), 'ECOA_BURN Programu ya upishi safi na bora, nchi mbali mbali' katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. PoA hii inasimamiwa na BURN Manufacturing Co.
Kwa muktadha huu, tunataka kuwakaribisha wadau wote wa ndani, walioathirika, na wale wanaopendelea, pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali, vikundi vya wanawake, taasisi za utafiti, na watu/washirika wanaofanya kazi katika masuala yanayohusiana na shughuli za mradi, wafanyabiashara wa sera za kitaifa na za kieneo, pamoja na watu wa kawaida, jamii, na wawakilishi ambao wanaweza kuathirika moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na mradi huu.
Kwa hiyo, BURN Manufacturing Co. (Ofisi ya Kuratibu na Kusimamia Mradi wa PoA) inawaalika wahusika wote kuhudhuria mojawapo ya mikutano ifuatayo ya Mashauriano ya Wadau wa Mitaa:
Tarehe 14 Machi 2022, saa 2:30 asubuhi - 7:00 mchana - Kilimanjaro Mhako Hostel & Restaurant, Usangi- Moshi
Tarehe 16 Machi 2022, saa 2:30 asubuhi - 7:00 mchana - Arusha Sharondi Bliss- Ulong’a Meru
Tarehe 18 Machi 2022, saa 2:30 asubuhi - 7:00 mchana - Dodoma Rafiki Dodoma Hotel- Dodoma
Wadau ambao hawawezi kuhudhuria mkutano kwa kufika ukumbini wanaweza pia kushiriki mtandaoni kupitia Zoom. Maelezo ya kuhudhuria mkutano mtandaoni ni kama ifuatavyo:
Tarehe 14 Machi Link: https://us02web.zoom.us/meeting/register/tZAlduqqqz4iGtKqP6ocCWQBtROgeFUzUey7
Tarehe 16 Machi Link: https://us02web.zoom.us/meeting/register/tZwkc-upqjgqGNRkJlssA8EVjpJTQR1AEuUL
Tarehe 18 Machi Link: https://us02web.zoom.us/meeting/register/tZwtd-GsqTwiG9NoJ2VX7n39i2krJHS8KfGs
Unaweza pia kupata muhtasari usio wa kiufundi wa mradi hapa kwa kumbukumbu yako.
Iwapo una maswali au unahitaji maelezo zaidi na habari kuhusu mradi kabla ya mashauriano, tafadhali wasiliana na Peninah Mwende, Afisa Kaboni wa BURN kupitia peninah.mwende@burnmfg.com.
Tafadhali tumia mawasiliano haya pia kuwasilisha maoni yako iwapo hutaweza kuhudhuria mkutano wa wadau.
RATIBA YA MKUTANO:
Tunatarajia kushiriki kikamilifu na kutoa maoni yako muhimu katika mradi huu wa kusaidia upishi safi na bora nchini Tanzania. Mchango wako ni wa maana katika juhudi zetu za pamoja za kukuza mazoea ya upishi safi na bora nchini Tanzania.